November 13, 2016

Eneo lililokumbwa na tetemeko la ardhi nchini New Zealand 

 Tetemeko kubwa la ardhi limepiga kisiwa cha Kusini mwa taifa la New Zealand.
Shirika la usoroveya wa maswala ya ardhini nchini Marekani limesema kuwa tetemeko hilo lenye ukubwa wa 7.4 katika vipimo vya Ritcher lilipiga eneo hilo mwendo wa saa sita usiku ikiwa ni kilomita 95 kutoka Christchurch.
Wizara ya ulinzi wa raia imewaonya watu wanaoishi mashariki mwa pwani ya kusini mwa kisiwa hicho kuhamia maeneo ya juu ili kujilinda dhidi ya Tsunami.
Eneo la ChristChurch bado linaendelea kujiponya kutoka kwa tetemeko la 2011 ambalo liliwaua takriban watu 185 na kuharibu eneo la katikati la mji huo.
Gazeti la Herald linasema kuwa mtingisiko wa tetemeko hilo ulisikika hadi Wellington ,ambapo ving'ora vilisikika huku raia wakiyatoroka makazi yao na kuelekea kwenye barabara baadhi yao wakilia.
Taifa la NewZealand lipo katika eneo linalokumbwa na matetemeko mengi ,milipuko ya volkano inayozunguka mduara wote wa eneo la Pacific.
Ripoti za awali zilisema kuwa baadhi ya nyumba katika mji wa Cheviot ,karibu na kitovu che tetemeko hilo zimeharibiwa.
Mkaazi wa Christchurch anasema kuwa tetemeko hilo lilifanyika kwa mda mrefu.
''Tulikuwa tumelala tukaamshwa na nyumba iliokuwa ikiyumba'' .

Chanzo:BBC Swahili.com

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE