December 05, 2016


Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi mkuu wa ACT Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe, ijumaa ya December 2 aliofanya ziara mkaoni Arusha . Katika ziara hiyo Ndugu. Kabwe alitembelea Chuo cha Kilimanjaro International Information Technology kwa malengo ya kuanzisha chuo kama kile Mkoani Kigoma. Zittoa ameandika hivi Facebook
Leo mchana ijumaa 2 December -  nilikuwa mkoani Arusha Kwaajili ya kutekeleza majukumu na kazi zangu kama Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini (Ujiji). Ziara yangu mkoani Arusha ilikuwa makhsus kwaajili ya kutembelea Chuo cha Kilimanjaro International Information Technology & Computing College (KIITEC).
Jimboni Ujiji tuna lengo la kuwa na chuo cha Ufundi cha namna hii, kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuwaongezea maarifa vijana wetu kupitia kozi mbalimbali zinazotolewa na vyuo vya aina hii. Nawashukuru sana KIITEC, nimejifunza, Ujiji tutajitahidi kuiga jambo hili zuri la watu wa Arusha.
Pia, nilipata fursa ya kumsalimu Mbunge mwenzangu wa jimbo la Arusha Mjini, ndugu Godbless Lema, gerezani Kisongo. Nimefurahi kumkuta akiwa na ari kubwa na asiyekata tamaa.
Ujumbe wake kwangu ni kuwa yeye yu tayari kukaa mahabusu kwa muda wote ambao Serikali itaona inafaa, na akaniasa nisimpiganie kwenye hili, bali nilitazame kwa upana kwa kuwa wapo watanzania wengi mno wanaokaa muda mrefu sana mahabusu kwa kesi ambazo wangeweza kupewa dhamana. Amenihimiza tujikite katika kuwatetea hawa. Ombi ambalo nimeahidi kwake kulitekeleza.
Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Arusha
Disemba 2, 2016

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE