January 25, 2017

 

Licha ya juhudi kubwa za wadau kutetea haki za watoto bado wazazi na walezi wengi wameshindwa kuhakikisha sauti za watoto zinasikilizwa ili waweze kutimiza ndoto zao. Katika kuhakikisha sauti za watoto zinasikilizwa Da Huu wa #LeoTena - Leo 25/01/2017 amefanya uzinduzi wa taasisi yake ya Dahuu Foundition ikiwa na lengo na dhamira ya kupaza sauti za watoto kusikilizwa kwa haraka zaidi

Image may contain: 30 people, crowd 
Wanafunzi wa shule ya msingi Ilala wakisikiliza kwa makini kwenye uzinduzi wa Dahuu Foundation iliyo chini ya mtangazaji wa kipindi cha #LeoTena, Husna Abdul 'Dahuu', yenye lengo la kuwasaidia watoto wa Tanzania kuwapa nafasi sauti zao kusikika na waweze kutimiza ndoto zao.
Dahuu amezindua Foundation hiyo, ikiwa leo ni siku yake ya kuzaliwa#HappybirthdayDahuuu #DahuuFoundation

 

‘’Dhumuni la shughuli hii leo, kwanza kabisa nazindua Taasisi yangu inaitwa #DahuuFoundation, kinachofanyika kwenya Foundation hii ni kuwasaidia watoto wa Tanzania kuwapa nafasi sauti zao kusikika, wazo hili limetokea kwenye kipindi chetu cha #LeoTena kupitia segment ya Hekaheka yamekuwa yakitokea matukio mengi ya kusikitisha na yamekuwa yakiniumiza sana, kwahiyo nilitafakari na kuamua kwenda mashuleni kuanzisha taasisi maaalum ambayo itakuwa ikitembelea shule hizo kutoa elimu kwa watoto na kuwapa nafasi ya kuwajengea uwezo tukiwa na wanasaikolojia wenye uwezo wa kuzungumza na mtoto, na kumdadisi na akaweza kueleza kama ananyanyasika, anapata matatizo na kuyaeleza kabla ya kufika hatua kubwa na kuwa heka heka’’ @dahuuofficial#UzinduziDahuuFoundation

 
Ushawahi kufikiria pindi watoto wanaposhuhudia matatizo wanayokumbana nayo wazazi wao au watu wao wa karibu nani huwa anahusika kuwashauri? 
Au mtoto anapokumbana na matatizo nani anamshauri ili kufanya arudi katika hali yake ya kawaida? 
Hapo ndipo umuhimu wa wanasaikolojia unapohitajika @auntsadaka akitoa neno kwa wanafunzi wa shule ya msingi Ilala kwenye uzinduzi wa #DahuuFoundation Ilala


MACHAKU MEDIA tunamtakia Dahuu kila la kheri katika harakati zake za kuikomboa jamii hasa ya watoto na kufikisha malengo yao yatimie. Happy Birthday Dahuu

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE