Dogo Mfaume enzi za uhai wake.
Kifo cha msanii wa muziki wa Mchiriku, Mfaume Selemani maarufu kama
Dogo Mfaume, kimekuja ikiwa ni siku chache tangu Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla kutoa
msaada kwa ajili ya matibabu ya uvimbe karibu na ubongo uliokuwa
unamsumbua.
Dogo Mfaume aliyewahi kutamba na wimbo ‘Kazi Yangu ya Dukani ‘,
amefariki leo (Jumanne) katika hospitali ya Taifa Muhimbili (MHN)
alipokuwa amelazwa akiendelea na matibabu.
Mmiliki wa kituo cha Pili Misana Back To Life sober house kinachotoa
matibabu kwa waathirika wa dawa za kulevya, Pili Misana amesema
Kigwangalla alitoa msaada huo baada ya fedha za matibabu kukosekana.
“Dogo Mfaume alikuwa akisumbuliwa na maradhi tangu mwanzoni mwa mwaka
huu na baadaye iligundulika kuwa na uvimbe karibu na ubongo na hapo
ndipo Naibu Waziri akatupatia msaada tukaanza matibabu Muhimbili,”
amesema.
Amesema wiki hii Dogo Mfaume alikuwa amelazwa Muhimbili akisubiri kufanyiwa upasuaji Ijumaa.
“Kesho tulitakiwa twende hospitali kwa ajili ya kumtolea damu, lakini kwa bahati mbaya amefariki,”amesema.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment