
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli,
amewaahidi wafanyakazi ujio wa nyakati za neema baada ya serikali
kukamilisha zoezi la kuwasafisha watumishi hewa, na kutangaza kutoa
ajira mpya 52,000 katika mwaka huu.
Rais
Dk. Magufuli ametoa kauli hiyo leo Mkoani Kilimanjaro katika sherehe
za Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) zilizofanyika
katika uwanja wa Ushirika, na kusema hadi sasa wameshabaini wafanyakazi
hewa 19,706.
Amesema
kuwa wafanyakazi hao walikuwa wakiingiza serikali hasara ya shilingi
bilioni 19.84 kwa mwezi zaidi ya shilingi bilioni 230 kwa mwaka, jambo
ambalo iwapo angeongeza mishahara watumishi hao hewa nao wangenufaika.
Rasi Magufuli akifurahia jambo wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani, ambapo Tanzania yamefanyika kitaifa Moshi. Kilimanjaro.
Rais Magufuli amesema katika bajeti ya mwaka ujao Serikali itaongeza nyongeza za mshahara ya wafanyakazi wa umma ya kila mwaka, pamoja na kuwapandisha madaraja wafanyakazi, jambo ambalo lilikuwa limesimama kwa muda kupisha zoezi la kusafisha wafanyakazi hewa na wenye vyeti feki
Aidha, Mhe, Dk. John Magufuli ameagiza mfanyakazi yoyote atakayehamishwa bila ya kupewa fedha zake za uhamisho asikubali kuhama, bila ya kupewa fedha hizo, na kuongeza kuwa kunawakati mwingine wafanyakazi wanahamishwa na maboss zao kwa kuonewa au kuonewa wivu tu.
"Sasa niwaombe wafanyakazi yoyote atakayekuhamisha hakuna kuhama mpaka ulipwe pesa zako, asipokulipa hakuna kuhama, ukiona anakwambia uhamiem sehemu anakupa na check yako hapo sawa wewe hama ila vinginevyo hakuna kuhama" alisema Rais Magufuli
0 MAONI YAKO:
Post a Comment