May 22, 2017

 
Baada ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe kuwataka wasanii wa muziki nchini kuacha kufanya muziki ambao una uhusiano na siasa, rapa Nay wa Mitego amefunguka kuhusu kauli hiyo na kutuma ujumbe maalum kwa waziri huyo.
Waziri huyo aliyasema hayo mwezi huu Bungeni wakati akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa na wabunge wakati wa kujadili hotuba ya Bajeti ya wizara yake.

Akiongea na Bongo5 Jumamosi hii, Nay amedai yeye ni mmoja kati ya wasanii ambao hawajaielewa kauli hiyo na mweshimiwa.

“Mimi sijawahi kuimba siasa huwenda hiyo kauli hainihusu, muziki wangu ni maisha ya watu ya kila siku, huwa siimbi siasa. Lakini nachoamini siasa pia ni maisha ya watu ya kila siku, muziki wa hip hop ni maisha ya watu ya kila siku na siasa ni maisha ya watu ya kila siku,” alisema Nay wa Mitego.

       

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE