
Msanii wa muziki wa Injili Tanzania, Emmanuel Mbasha amefunguka kwa
kudai kuwa hana tatizo na mwanaume ambaye amemuoa aliyekuwa mama watoto
wake, Flora.
Muimbaji huyo amedai hata akikutana na mwanaume huyo hawezi kumfanya
lolote maana huyo mtu hakuwahi kumuingilia katika ndoa yake.
“Jamaa ambaye amemuoa Flora sina shida naye, anaweza kuwa mtu ambaye
ananihofia kuwa nikikutana naye naweza kumdunda,” alisema Mbasha.
Aliongeza, “Ila huyo jamaa mimi simchukii na wala simjui. Hajawahi
kuniingilia kwenye issue yangu yoyote ya mapenzi ila mimi namchukia
jamaa ambaye aliniingilia kwenye ndoa yangu ndiye mbaya wangu, na
Watanzania wote wanamjua,”
Mbali na hilo Emmanuel Mbasha alisema kuwa Flora amemkimbia kutokana
na maisha aliyoyachagua lakini si kwamba alikuwa hana pesa, kwani yeye
pesa alikuwa nazo toka mwanzo.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment