Nimekuwa naulizwa Sana kuhusu uteuzi wa Mwenyekiti wa Chama chetu kuwa
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Nimekuwa kimya Kwa sababu tumepokea Taarifa
za uteuzi kutoka katika vyombo vya Habari. Mwenyekiti yuko nje ya nchi
na kutokana na tofauti za masaa bado hatujawasiliana nae. Tutatoa tamko
kamili atakapokuwa amerejea nchini.
Ninawataka wanachama wote wa Act Wazalendo wawe watulivu na Kama kuna
masuala yanayohusu maamuzi ya vikao vya Chama tutawajulisha.
Aliyeteuliwa ni Mwenyekiti wa Chama Taifa, sio mshauri au mwanachama tu.
Ni mmoja wa viongozi wa juu wa Chama chetu. Uteuzi wake unahitaji kikao
cha Kamati Kuu ya Chama kukaa na kujadili. Nitaweza kutoa Taarifa baada
ya vikao vya Kamati Kuu ya Chama. Kwa sasa umma usubiri vikao Kwa
mujibu wa Katiba ya Chama chetu.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment