Filamu ya ‘All Eyes On Me’ iliyotengenezwa kwa ajili ya kuonesha maisha
halisi ya marehemu Tupac Shakur itaanza rasmi kuonekana leo kwa watu.All Eyes On Me’ iliyozinduliwa jana na hatimaye siku ya leo kupitia
kituo cha runinga cha HBO itaanza kuruka, Filamu hiyo ilianza
kutengenezwa tangu mwaka jana katika miji mbali mbali ikiwemo Altanta,
Sin City na mingineyo nchini Marekani huku ikiwa chini ya mtayarishaji,
L.T. Hutton.
Kijana aitwaye Demetrius Shipp Jr. ameigiza katika filamu hiyo kama
Tupac huku Danai Gurir akiigiza nafasi ya Afeni Shakur ambaye ni mama
mzazi wa rapper huyo ambaye alifariki mwezi Mei, mwaka jana.
Tupac alipigwa risasi baada ya kutoka katika pambano la ndondi kati
ya Mike Tyson na Bruce Seldon, Septemba 7, 1996. Na alifariki dunia
Septemba 23 mwaka huobaada ya kupoteza damu nyingi.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment