Awali Mwenge huo ulipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo ,Alhaj Majid Mwanga ukitokea Kibaha, ambapo katika Wilaya hiyo ya Bagamoyo uliweza kutembelea miradi yenye thamani ya zaidi ya sh .bilioni 128.
Aidha kwa Halmashauri ya Chalinze Mwenge huo uliweza kutembelea miradi Tisa ambapo wamejipanga kuinua uchumi na kupiga maendeleo kupitia viwanda na fursa mbalimbali za kiuzalishaji.
Mwenge huo wa Uhuru uliweza kulala katika Halmashauri hiyo ya Chalinze na unakabidhiwa Mkoa wa Morogoro leo.
Mkuu
wa wilaya ya Bagamoyo , Alhaj Majid Mwanga akipokea Mwenge wa Uhuru
kutoka wilaya ya Kibaha, Awali wakati wa Mwenge huo ulipowasili wilayani
humo.
Baadhi
ya Wananchi wa Halmshauri ya Chalinze wakiwa kwenye mkusanyiko wa
Mwenge ambao ulilala hapo kabla ya leo Asubuhi kupelekwa kukabidhiwa
Morogoro
Baadhi
ya Wananchi wa Halmshauri ya Chalinze wakiwa kwenye mkusanyiko wa
Mwenge ambao ulilala hapo kabla ya leo Asubuhi kupelekwa kukabidhiwa
Morogoro
Majira ya Asubuhi Mwenge huo ukiendelea na majukumu ya kutembelea miradi mbalimbali katika Halmashauri hiyo ya Chalinze.
Baadhi
ya viongozi na wakimbiza Mwenge wakiwa katika moja ya viwanda katika
Halmashauri ya Chalinze wakati Mwenge Uhuru ulipotembelea miradi hiyo
leo Juni 10.2017
Mbunge
wa jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwani Kikwete akipata maelezo ndani ya
moja ya viwanda ndani ya Halmashauri ya Chalinze wakati Mwenge huo
ulipotembelea kukagua miradi mbalimbali.
Mbunge
wa jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwani Kikwete akiwa pamoja na baadhi ya
viongozi wa Halmashauri ya Chalinze na Wilaya hiyo ya Bagamoyo wakati wa
Mwenge huo ukitembelea miradi mbalimbali kwenye Halmashauri hiyo.
Mwenge huo unatarajia kukabidhiwa Mkoa wa Morogoro leo Juni 10.2017.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment