Tende ni tunda ambalo linayeyuka kirahisi tumboni na lenye faida nyingi sana ambazo hulifanya liwe tunda la kipee.
Zifuatazo ni faida ya tunda la tende katika mwili wa binadamu.
Kwa watu wenye matatizo ya tumbo, nicotinic inayopatikana kwenye tende
husaidia kurekebisha matatizo ya tumbo na huleta ahueni kwa watu wenye
matatizo ya kupata choo.
Tende husaidia kuuimarisha moyo. Iloweke tende kwenye maji kwa usiku
mmoja na asubuhi kunywa maji hayo pamoja na tende zilizolewekwa baada ya
kuondoa mbegu, ukifanya hivyo mara mbili kwa wiki, moyo wako utakuwa
imara.
Tende husaidia pia kwenye mambo ya malavi davi. Iloweke tende kwenye
maziwa ya mbuzi usiku, asubuhi changanya maziwa hayo na asali kisha
kunywa, njia hii husaidia kuongeza nguvu na stamina.
Utafiti umeonyesha kuwa tende husaidia kutanua misuli ya mji wa mimba
wakati mwanamke anapokaribia kujifungua, hii husaidia kumfanya mwanamke
asipoteze damu nyingi wakati wa kujifungua.
Wataalamu wa vyakula, wanazichukulia tende kama chakula bora kwa
wanawake wanaonyonyesha kwani husaidia kuyapa maziwa virutubisho muhimu
vinavyomfanya mtoto awe na afya njema.
Tende husaidia kupunguza kiwango cha kilevi (alcohol) kwenye damu. Maji
ya kunywa ambayo tende imelowekwa ndani yake husaidia kuondoa haraka
alcohol mwilini.
Tende husaidia kuchelewesha dalili za uzee na pia husaidia kurekebisha ngozi na huondoa mabaka ya kuungua na jua.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment