
Mtoto wa rapper Future na mwanamuziki Ciara, Zahir Wilbur ambaye kwa
sasa analelewa na mama yake pamoja na baba yake wa kambo Russel Wilson,
amepata dili lake la kwanza la kuingiza fedha nyingi.
Zahir ambaye ana umri wa miaka mitatu amepata dili la kampuni ya Gap
Kids ambapo atakuwa akihamasisha watoto kupelekwa shuleni. Ciara kupitia
mtandao wa Instagram, ameonyesha kufurahi mafanikio hayo aliyoanza
kuyapata mtoto wake.

0 MAONI YAKO:
Post a Comment