Kikosi cha Polisi Moro

Afisa habari wa timu ya Polisi Tanzania Frank Geofrey akihojiwa na Mwandishi wa habari hizi jana

Afisa habari wa timu ya Polisi
Tanizania Afande Geofrey akiwa na Afisa habari wa Jeshi la Polisi Mkoa
wa Morogoro Afande Mohamed Ngwaya
TIMU yasoka ya Polisi Morogoro ambaye kwa
sasa inajulikana kwa jina la 'Polisi Tanzania' imeamua kuondoka Mkoani
Morogoro na kuhamia Moshi Mkoa wa Kilimanjaro.
Taarifa za kuhama kwa Maafande hao
zilizagaa jana kwenye Mjini hapa wakati timu hiyo ilipokuwa wakionyesha kazi na timu ya Mawenzi Market yenye maskani yake
Soko la Matunda la Mawezi lililopo kata ya Kiwanja cha Ndege Manispaa ya
Morogoro.
Kufuatia kuzagaa kwa habari hiyo
Mwandishi wa Mtandao huu aliamua kumvaa Afisa habari wa timu hiyo
Afande Frank Geofrey ambapo alipotakiwa kuzungumza madai hayo
alithibisha kwa kusema.
"Ni kweli timu yetu inahamia Moshi na
kuanzia gemu iyajo ambayo tutacheza na Mbeya kwanza tutacheza kwenye
uwanja wetu wa nyumba wa Chuo Cha Ushirika Moshi" Alisema Afande huyo Geofrey
Na Dustan Shkidele
0 MAONI YAKO:
Post a Comment