Shilole msanii wa muziki na filamu wa Tanzania.
Msanii Shilole ameweka wazi kile ambacho watu wengi walikuwa hawafahamu
kuhusu watoto wake, na kusema kwamba mambo yake ya mitandaoni
hayawaathiri na badala yake wako vizuri darasani huku mmoja wao akiwa na
ndoto kubwa ya kugundua dawa ya UKIMWI
Akizungumza
na mwandishi wa habari Shilole amesema pamoja na kwamba yeye hajapata
bahati ya kusoma, lakini watoto wake wako makini na shule huku akiwaonya
na kuwasisitiza kuwa makini, kwani iwapo watafanya vibaya watakuwa
wanamuangusha kutokana na anayoyapitia kwa ajili yao, hivyo wanazingatia
ipasavyo kauli ya mama yao na kutojihusisha na mambo ya mahusiano yake.
"Wanangu hawana shobo na haya mambo, wanataka niwe na furaha, ndio
maana hujaona watoto wangu wameniangusha kwenye masomo kwa vitu vya
kusikia kwenye mitandao, ndio kwanza wanaongoza namba moja, namba mbili,
nawaambia mkifanya blanda mnaniangusha mimi, mkifanya tukio mjue
mnanizika, kwa hiyo watoto wangu wapo makini na masomo kuliko kitu
chochote, huyu mmoja anasoma aje kuwa dokta ili aje agundue dawa ya
UKIMWI, kwa nini uliletwa, na anafanya vizuri darasani", alisema
Shilole.
Shilole ambaye ana watoto wawili wote wakiwa wa kike, anasema
anajisikia faraja kuona watoto wake wanapa fursa ya kufanya yale ambayo
yeye hakufanikiwa kuyafanya, ikiwemo kupata elimu bora ambayo anaamini
itakuja kuwasaidia baadae kwenye maisha yao.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment