
Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniphace Jacob amefunguka na kusema kuwa
hawezi kufuta kesi yake dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhusu
sakata la vyeti feki na kusema anataka kuona kesi hiyo inafanyika kwa
uwazi ili watu wote wajue kinachoendelea
Boniphace Jacob amesema hayo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa
habari baada ya kutoka kwenye Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa
Umma na kusema yeye dhamira yake jambo hilo liweze kufika kwenye baraza
la maadili ambalo litakuwa ni wazi na watu kusikia na kuona kila jambo
ambalo litakuwa likiendelea.
"Mbaka steji hii hakuna
jambo ambalo tumeambiwa limepingwa kwa vielelezo kutokana na jinsi
alivyoambiwa ajielezee juu ya vyeti feki, kitu tunachopigania sasa ni
kwenda kwenye baraza la mwisho la maadili ambalo ni la wazi ambapo
tutamuhoji kwa kila kitu ambacho anatuhumiwa nacho, kwa hiyo kama mimi
ndiyo natuhumiwa kwa vyeti nitavitoa hadharani kumuonyesha jaji na watu
wote wataruhusiwa kuviona" alisema Meya Boniphace
Aidha Meya huyo amesema kuwa kitendo cha yeye kuambiwa kuwa amtafute Mkuu wa Mkoa kabla ya jambo hilo halijafika kwenye baraza la maadili anaona jambo hilo limefungua vitisho kwake na mazingira ya ushawishi wa rushwa na kusema hiyo kwake si dhamira yake bali yeye atapenda hilo jambo lifike kwenye baraza la maadili ili kila mtu aweze kufahamu mambo hayo.
"Kitendo cha kumwambia kwamba anitafute tumalizane ili tusifikwe kwenye baraza la maadili binafsi naona limefunguka vitisho na vishawishi ambavyo kimsingi si dhamira yangu mimi nimependa shauri langu toka mwanzo lianze kwa uwazi na liishe kwa uwazi. Kwa hiyo natangazia umma na yeye mwenyewe asikie kuwa mimi dhamira yangu nikiwa hai au nikiwa nimekufa nataka shauri hili lifike kwenye baraza la maadili jambo hili likaendeshwe kwa uwazi na kila mtu ashuhudie" alisema Meya Jacob
0 MAONI YAKO:
Post a Comment