Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Abdulrahman Kinana
amefuta mchakato wa kura za maoni za kumtafuta mgombea ubunge kupitia
chama hicho katika jimbo la Singida Kaskazini baada ya kugundua kuwa
kuna viashiria vya rushwa kwa wagombea wa nafasi hiyo.
Ndg. Kinana amewasimamisha kabisa wagombea wawili, Haider Gulamali na
Elia Mlangi kutojihusisha na mchakato huo tena wa kura za maoni na kwa
mabadiliko hayo mchakato wa kura za maoni utaanza upya kesho ambapo watu
wenye nia ya kugombea watahitajika kuchukua fomu na kujaza kisha
kuzirudisha. Jimbo la Singida Kaskazini limekuwa wazi tangu Mhe. Lazaro Nyalandu
ajivue uanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mwishoni mwa mwezi Oktoba
mwaka huu. Soma zaidi:
0 MAONI YAKO:
Post a Comment