Wanachama wa chama cha Social Democrats (SPD) cha Ujerumani wameridhia chama chao kujiunga kwa mara nyingine tena katika serikali ya mseto na muungano wa vyama vya kihafidhina - Christian Democratic Union (CDU) cha Kansela Angela Merkel na Christian Social Union (CSU), baada ya matokeo ya kura zilizopigwa kwa njia ya posta, zilizoonesha kuwa wameridhia kwa asilimia 66. Matokeo hayo ya kura yatafungua njia kwa serikali iitwayo Muungano Mkuu kati ya SPD, CDU na CSU, ambao umeongoza nchini Ujerumani tangu mwaka 2013. Vile vile, uamuzi huu wa leo unahitimisha mkwamo wa kisiasa wa takribani miezi minne katika taifa lenye nguvu zaidi kiuchumi barani Ulaya.
MCHENGERWA: BIMA YA AFYA KWA WOTE IWE KIPAUMBELE BAJETI YA 2026/27
-
Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa akizungumza kwenye ufunguzi wa kikao cha
baraza kuu la wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika jijini Mwanza.
Waziri w...
5 hours ago






0 MAONI YAKO:
Post a Comment