Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza kuanzisha vipindi vya michezo
vitakavyo ruka katika luninga ya Azam TV kama ilivyo kwa mahasimu wao
Simba SC ambao wao tayari walishaanza pamoja na timu ya Azam FC.
Wakiongea na waandishi wa habari katibu mkuu wa klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa na meneja wa vipindi wa Azam Tv, Baruani Muhuza wamesema
kuwa vipindi hivyo vitakuwa na utafauti mkubwa na vile vya klabu za
Simba na Azam FC kwakuwa vitakuwa vikizalishwa katika studio za hapo
klabuni na kunamatarajio ya kuanzisha na kituo cha radio.
Yanga inatarajia kuzindua rasmi vipindi hivyo vya michezo ambavyo
vitakuwa vikizalishwa hapo makao makuu Jangwani mwezi ujao na hivyo
watangazaji watakuwa ni wana Yanga wenyewe.
Wakati huo huo uongozi ya wanajangwani hao umeingia mkataba na
mtandao wa simu za mkononi Tigo ambao watawezesha wanayanga na wapenzi
wa soka kwa ujumla kupata habari kupitia ujumbe mfupi wa njia ya simu
‘SMS’.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment