April 26, 2018

 

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu tisa waliokuwa wakiandamana eneo la Samora Avenue Posta, Dar es Salaam.Kamanda wa Polisi Kanda, Lazaro Mambosasa amethibitisha kukamatwa kwa watu hao. Kukamatwa kwao kumekuja mara baada ya Jeshi la Polisi kuonya kuwa litawachukulia hatua kali wale wote watakaokaidi agizo la kutoandamana kama walivyoagiza.
Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi mkoani Iringa linamshikilia kwa mahojiano Diwani wa Kata ya Igumbiro, Musa Mlawa kwa kosa la kufanya mkusanyiko usio halali.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire Diwani huyo anashikiliwa kwa mahojiano ili kubaini chanzo cha mkusanyiko huo.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE