
Mona akiwa na mpinzani wake Lupita Nyongo toka Kenya
Mrembo na muigizaji mkongwe kwenye tasnia ya filamu nchini Yvonne
Cherrie maarufu kama 'Monalisa' ameibuka mshindi kwenye tuzo za 'The
African Prestigious Awards' nchini Ghana akimbwaga mpinzani wake Lupita
Nyong'o.
Katika tuzo hizo zilizotolewa usiku wa kuamkia leo huko jijini Accra
nchini Ghana Monalisa ametwaa tuzo katika kipengele cha 'Best African
Actress'. Kwa mujibu wa tuzo hizo Monalisa sasa ndiye muigizaji bora wa
kike barani Africa.

Monalisa amethibitisha ushindi wake kupitia mtandao wa 'Instagram'
ambapo amepandisha picha akiwa na tuzo yake na kuandika ujumbe huu
''Tumeshindaaaaaaa narudi home na Tuzo za kutosha.Ahsante
Watanzania,Nawapenda mno''.
Kwa ujumbe huo wa Monalisa unaashilia huenda pia kuna tuzo nyingine
wameshinda Watanzania ambao walikuwa wanawania vipengele mbalimbali
katika tuzo hizo kubwa za filamu nchini Ghana.
Watanzania wengine waliokuwa wanawania ni King Majuto kipengele cha
Mchekeshaji Bora Afrika, Vicent Kigosi kipengele cha msanii Bora wa
Kiume Afrika na Mpiga picha Mahiri Moiz Hussein katika kipengele cha
Mpiga Picha Bora Afrika.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment