May 15, 2018

 Image result for Wizara ya Mambo ya Ndani
Muigizaji wa filamu nchini, Elizabeth ‘Lulu’ Michael ameanza kutumikia kifungo  chake cha nje Mei 15, 2018 kama moja ya masharti aliyopewa baada ya kuachiwa kutoka gerezani jana.

Lulu akiwa na wenzake 10 wamepangiwa kufanya usafi katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani zilizopo Posta Jiji la Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa maelezo kutoka  Mkurugenzi wa Probesheni na Huduma za jamii, Charles Nsanze amesema kila siku mwigizaji huyo atatumia saa nne kusafisha mazingira kisha ataendelea na shughuli zake nyingine za ujenzi wa taifa.
Atapumzika siku za Jumamosi na Jumapili au siku za sikukuu, hatakuwa peke yake kwa kuwa tayari hapa wapo wafungwa wengine tisa wanaofanya kazi za usafi wa mazingira.” amesema Nsanze kwenye mahojiano yake na gazeti la Mwananchi.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE