
Na Said Mwishehe,Blog ya jamii
BARAZA la Mitihani la Tanzania(Necta) limetoa onyo kali kwa wamiliki
wa shule,walimu na wananchi kutojihusisha na vitendo vya udanganyifu wa
mitihani ya Kidato cha Sita na Kozi za ualimu inayoanza kesho Mei 7 hadi
Mei 25 mwaka huu.
Kwa mujibu wa baraza hilo ni kwamba jumla ya watahiniwa 87,643
wamesajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha sita ambapo kati yao
watahiniwa wa shule ni 77,222 na watahiniwa wa kujitegemea ni 10,421.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji wa Necta
Dk.Charles Msonde ametangaza kuanza kwa mitihani hiyo ambapo ameonya
watu kutojihusisha na udanganyifu wa aina yoyote.Akisisitiza Dk.Msonde
amesema baraza la mitihani halitasita kumchukulia hatua yeyote
atakayejihusisha kufanya udanganyifu katika mihitani kwa mujibu wa
kanuni za utumishi wa umma na sheria za nchi.
Amefafanua ikiwa panoja na kuwafutia matokeo yote watahiniwa
watakaobainika kujihusisha na vitendo vya udanganyifu."Wadadau wore
wanaombwa kutoa taarifa katika vyombo husika kila wanapobaini uwepo wa
mtu au kikundi cha watu kujihusisha na udanganyifu wa mitihani wa aina
yoyote ile," amesema Dk.Msonde.Pia amesema baraza linatoa mwito kwa
jamii kutoa ushirikiano katika kuhakikisha mitihani hiyo inafanyika kwa
amani na utulivu .
"Wananchi wanaombwa kuheshimu eneo la mitihani na kuhakikisha
asiyehusika haingii maeneo ya shule,"amesema Dk.Msonde.Ameongeza
wamiliki wa shule na vyuo wanatakiwa kutambua shule na vituo vya maalum
vya mitihani na hivyo hawatakiwi kwa namna yoyote kuingiliwa majukumu
ya usimamizi wa mitihani kwa kipindi chote hicho.
" Baraza halitosita kukifuta kituo chochote cha mtihani endapo
litajiridhisha kuwa uwepo wake ubahatarisha usalama wa mitihani ya
Taifa,"amesema Dk.Msonde.Ametumia nafasi hiyo kutoa mwito kwa kamati za
mitihani za mikoa na halmashauri kuhakikisha taratibu zote za uendeshaji
mitihani ya Taiga zinazingatiwa ipasavyo.
Kwa upande wa wawatahiniwa ,amesema baraza linaamini walimu
wamewaandaa vizuri katika kipindi chote cha elimu ya sekondari na kozi
za mafunzo ya ualimu.Hivyo matarajio yao watahiniwa watafanya mitihani
yao kwa kuzingatia kanuni za mitihani ili matokeo yaoneshwe uwezo wao
halisi kulingana na maarifa na ujuzi walioupata kipindi cha mafunzo yao.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment