Mbunge wa Singida Mashariki @tundulissutz ,anatarajiwa kufanyiwa
oparesheni ya mwisho siku ya jumatatu. Katika ukurasa wake wa Instagram
Mh:Lissu anaandika kwa kutoa taarifa kwa watanzania
"Hello wapendwa wangu.
Ninaamini wengi wenu, kama sio wote, mnafahamu kwamba Jumatatu tarehe 4 June nitafanyiwa operesheni ya mwisho kwenye mguu wa kulia. .

Ni operesheni kubwa
inayotazamiwa kuchukua takriban masaa nane kwa taarifa nilizopewa tangu
mwanzoni mwa wiki hii. Hivyo madaktari wangu wametumia muda mrefu kidogo
kuniandaa kwa ajili ya Jumatatu. .
Napenda niwajulishe kwamba ninajisikia vizuri kiafya, na baada ya kuangikwa kitandani tangu tarehe 11 Aprili niliyofanyiwa operesheni ya pili, sasa niko tayari kwa ajili ya hii ya mwisho. Madaktari wangu wako vizuri. Nina imani watafanya kazi nzuri ya kitabibu. .
Kwa ninyi marafiki na ndugu zangu. Mmekuwa na mimi na familia yangu tangu tarehe 7 September ya mwaka jana. Mmetusaidia kwa maombi na kwa majitoleo yenu ya hali na mali. Bado safari ni ndefu lakini ninaweza kusema nimeanza kuona mwanga katika hili tanuru refu. .
Nimesema mara nyingi kwamba ninaona fahari na faraja kwamba Watanzania wenzangu na wasio Watanzania wamenitibu na wanaendelea kunitibu. Najua mtaniponya kwa nguvu za Mola wetu na kwa upendo na ukarimu wenu. Nawaombeni msichoke. .
Nawashukuruni sana"

0 MAONI YAKO:
Post a Comment