Rasmi Cristiano Ronaldo ajiunga na Juventus ya Italia
Imekuwa ni wiki yenye furaha kwa Mreno, Cristiano Ronaldo baada ya
kuvuta mkwanja mrefu kutoka klabu ya Juventus wakati mashabiki wa
vibibi hao wa Turin wakimiminika kununua jezi za staa huyo.
Jezi halisi ya Ronaldo ambayo imetengenezwa na klabu ya Juventus ambazo ni za mechi za nyumbani zinagharimu kiasi cha dola 144.95 ambayo ni sawa na Tsh 329715.16.
Jezi hiyo hiyo ya nyumbani kwa upande wa wanawake inagharimu kiasi cha dola 94.95 ambayo ni sawa na Tsh 215977.78
Ronaldo mwenye umri wa miaka 33, ameingia kandarasi ya pauni milioni 105 kutua Juventus siku ya Jumanne akitokea Real Madrid.
Ronaldo
alikutana na rais wa timu ya Juventus, Andrea Agnelli mchana wa siku ya
Jumanne kwenye hoteli huko Greece ambapo alikuwa mapumzikoni na mpenzi
wake pamoja na familia kabla ya kukubali dili hilo la miaka minne ambalo
atavuna kiasi cha pauni 500,000 kwa wiki.
Hapo
jana siku ya Alhamisi nyota huyo ameonekana akifurahia maisha na
familia yake akiwa sambamba na marafiki zake akiposti picha kwenye
instagram inayo muonyesha akipata chakula cha usiku.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment