Mwandishi wa habari hizi alikutana na msanii huyo kwenye moja ya maeneo tata ambapo alianza kutoa maneno kuwa tayari ameshatulizwa nguvu na mmoja wa wanaume ambaye hata hivyo hakutaka kumtaja jina.
Alisema kuwa ujauzito huo una mwezi mmoja na hafikili kitu kibaya eti kuutoa kama baadhi ya wasanii walivyo na tabia chafu ambayo ni dhambi kubwa kwa mungu.
Alisema kuwa anapenda mtoto kwani hata hivyo huyo atakuwa mtoto wake wa pili kwani wa kwanza yupo na ana miaka 7.
“Mimba hii haitakuwa ya kwanza kwangu hivyo naelewa nini maana ya kulea hivyo nawapa soma wasanii ambao hawataki kuzaa kwamba kuwa na mtoto raha tupu,” alisema.
Hata hivyo msanii huyo alitoa siri ya baadhi ya nyota wanaotoa mimba ni kwamba wanajua wakishaonekana wana mimba watakosa soko mjini na hata baadhi ya wanaume wataanza kuwa kimbia.
Kwa upande wake aliongeza kuwa haoni tatizo kushika mimba kwani maisha yake anayaendesha mwenyewe ingawa wanaume wapo na hawatoisha.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment