April 28, 2024


Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe, Dkt. Abdulaziz M. Abood ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kugawa vizimba katika Soko la Machinga Complex lililopo maeneo ya FIRE  kwa watu na wafanyabiashara waliokusudiwa na ambao wanahitaji vizimba hivyo ili kukuza na kuboresha mitaji ya wafanyabiashara wadogo.

Mhe Abood ametoa kauli hiyo katika shughuli za uwekaji wa jiwe la Msingi kwenye Soko hilo Aprili 27 Mwaka huu mbele ya kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru ndugu Godfrey Mzava, wakati Mwenge, ulipotembelea Mradi huo kwa ajili ya kuukagua na kujionea maendeleo ya Mradi hadi uliopofikia.

Mhe Abood ameweka wazi kuwa, Mradi huo umegharimu kiasi cha shilingi Mil. 696, fedha ambazo zimetokana na mapato ya ndani ni kiasi cha Shilingi Mil. 199 na kiasi cha shilingi Mil. 497 zimetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kujenga Soko hilo ili kuondoa kero kubwa iliyokuwa inawakabili wafanyabiashara wadogo wadogo waliokuwa wakiuza bidhaa zao kwa kutangatanga mitaani na kando kando ya barabara na sasa wawe na eneo maalum na lenye uhuru kwa ajili ya kuendesha biashara hizo.

Aidha, Mhe Abood amekemea tabia za baadhi ya watumishi ambao inapofika wakati wa kugawa vizimba kwa ajili ya wafanyabiashara hao, huchukua wao kisha kuwapangisha wenye mahitaji stahiki, jambo ambalo linaongeza chuki baina ya wananchi na Serikali yao, hivyo ili kuepukana na hilo Mhe Abood ametaka Vizimba hivyo kugawiwa kwa  waliolengwa na waweze kufanyabiashara ili kujikimu Maisha yao na familia zao.

“Wakati unapofika wa kugawa vizimba vya Soko hili, nashauri tuzingatie walengwa kwanza kwa sababu hadi kujengwa kwa Soko hili wao ndio kipaumbele, kwani wao ndo wanaoteseka na kutangatanga barabarani hadi Mhe Rais amewaona na kuamua kutoa fedha ili kujenga Soko hili. Tusije tukawapa watu wasiostahili halafu wakawapangisha wahitaji” Amesema Mhe Abood.

Kwa upande wake kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru amekagua Jengo la Soko hilo na kuridhishwa na maendeleo ya mradi huo, hivyo kuamua kuliwekea jiwe la Msingi la ujenzi wa Soko hilo, amesisitiza kuwa miradi yote ya kimaendeleo ambayo Rais Samia anatoa fedha ili kukamilisha miradi, lazima miradi hiyo isimamiwe kikamilifu kama ambavyo mradi huu umesimamiwa vema.
Katika hatua nyingine, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru ametembelea Kituo cha watoto wenye mahitaji maalum cha Mihayo kilichopo Kata ya Mazimbu ambapo Mwenge huo umetoa zawadi ya matihaji ya kibinadamu kama Mchele kg 250, Unga wa Sembe kg 100, Sukali kg 75, Unga wa Ngano kg 50, Maharagwe kg 50, Mafuta ya kupikia lita 60, Sabuni ya mche katoni 1, Chumvi katoni 1, Mbuzi 1, Sabuni ya unga kg 15, Tisheti pamoja na Mashuka 13.

Naye Mhe Rebeka Msemwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, amemuhakikishia Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru ndugu Godfrey Mzava kuwa, wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro wanamshuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwaletea fedha zaidi ya Bil. 3 ambazo zimeweza kuzalisha miradi ya kimaendeleo ambayo imepitiwa na kukaguliwa na Mwnge wa Uhuru katika Manispaa hiyo.

Sanjari na hayo, Mwenge wa Uhuru umefanikiwa kuzindua Shule mbili zilizojengwa wa Mradi wa Boost kutoka Serikali Kuu, Shule moja ya Msingi iitwayo Viwandani  iliyopo Kata ya Mafisa ambayo watoto wameshaanza kusoma na ujenzi wake umekamilika kwa 100%, na ya pili ni Shule ya Sekondari ya Mkundi Mlimani ambayo nayo pia imezinduliwa leo kupitia Mbio za Mwenge huo.

Imetolewa na: Kitengo cha Habari na Mawasiliano Ofisi ya Mbunge

August 07, 2022

 Kwenye Refresh ya Wasafi Tv, Dee amekazia kuwa siku zote wanawake wanajua Marioo anataka nini, hivyo mpenzi wake Janjaro amejua Jamaa anapenda viatu,nguo mpya na kusafiri na ndicho anacho kifanya hadi Dogo Janja kasahau kitu kinaitwa muziki.😁



 


Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imewafungulia mashtaka ya kimaadili Rais wa Yanga, Mhandisi Hersi Said na aliyekuwa Ofisa wa Klabu hiyo Haji Manara “Kamati ya Maadili ilimfungia miaka miwili Manara kujihusisha na shughuli yoyote ya mpira wa miguu lakini ameshindwa kutekeleza adhabu hiyo”


Kamati imesema Hersi amefunguliwa mashtaka kwa kwenda kinyume na ibara ya 16(1) (a) ya Katiba ya TFF pamoja na ibara ya 1(6) ya Katiba ya Yanga.

Taarifa ya TFF:
Baada ya Manara kuadhibiwa na Kamati ya Maadili ya TFF, Sekretarieti ilimwandikia barua Mhandisi Said kuhakikisha Klabu yake inaheshimu uamuzi huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili tayari amepelekewa mashtaka hayo, walalamikiwa watapewa mashtaka na mwito mara baada ya Kamati kupanga tarehe ya kusikiliza mashtaka hayo”.
ImageImage 
  KUMBUSHO LA HARAKA! Mwaka jana mlipoteza mechi siku ya mwananchi, lakini mliendelea kushinda michezo yote mbele na kutwaa vikombe vyote nchini. Ilinisikitisha sana kiasi kwamba wakati mwingine nikienda kwenye kidimbwi na kuomba kikombe kwa ajili ya kinywaji changu,

 

Karibu mpenzi wa Machaku Media katika kurasa za Magaazetini leo hii. Leo ni siku ya jumapili 07 August 2022. Tumekukusanyia baadhio ya kurasa za Magazetini zilizotufikia katika Meza yetu hapa STUDIO. Kwa taarifa za kina katika kurasa za Magzetini, fika katika Meza iliyo karibu nawe ujipatie nakala yako sasa.

 









 

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akimkabidhi cheti cha pongezi Mkurugenzi Msaidizi wa Kuzuia Ujangili, Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw.Robert Mande (kulia) kwa kushiriki katika utoaji mafunzo ya kukabiliana na ujangili na usafirishaji haramu wa mazao ya wanyamapori na mimea ndani na nje ya Bara la Afrika uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akifunga mafunzo ya siku tano ya kukabiliana na ujangili na usafirishaji haramu wa mazao ya wanyamapori na mimea ndani na nje ya Bara la Afrika uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Msaidizi wa Kuzuia Ujangili, Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw.Robert Mande (kulia) akizungumza na washiriki wa mafunzo ya kukabiliana na ujangili na usafirishaji haramu wa mazao ya wanyamapori na mimea ndani na nje ya Bara la Afrika uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akimkabidhi cheti cha pongezi Afisa Uwajibikaji na Mkurugenzi wa Haki wa Taasisi ya Grace Farm Foundation Rob Khattabi (kulia)kwa kushiriki katika utoaji mafunzo ya kukabiliana na ujangili na usafirishaji haramu wa mazao ya wanyamapori na mimea ndani na nje ya Bara la Afrika uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Kuzuia Ujangili, Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw.Robert Mande (kushoto) 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kukabiliana na ujangili na usafirishaji haramu wa mazao ya wanyamapori na mimea ndani na nje ya Bara la Afrika uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku tano ya kukabiliana na ujangili na usafirishaji haramu wa mazao ya wanyamapori na mimea ndani na nje ya Bara la Afrika wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (hayupo pichani)akifunga mafunzo hayo leo jijini Dar es Salaam.

June 21, 2021

January 29, 2020

 


Brand New Song kutoka kwake mwanamuziki Strevol toka mkoani Morogoro akimshirikisha MR. Blue toka jijini Dar. Wimbo umefanyika katika studi za Kwanza Records chini ya Producer Vennt Skillz

January 16, 2020


Kutokea mkoani Morogoro, producer Vennt Skillz, ameachia wimbo wake unaitwa Caribbean Girl

Download sasa

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe. Abdulaziz Abood (CCM) akiangalia namna mashine ya X-ray ya kisasa inavyofanya kazi katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.

Kufuatia kilio cha muda  mrefu cha wakazi wa  mkoa wa Morogoro juu ya kukosekana kwa mashine ya X-ray ya kisasa katika hospitali ya rufaa ya mkoa huo hali iliyokuwa ikiwalazimu kupewa rufaa kwenda hospitali ya taifa Muhimbili kwa ajili ya Matibabu hatimaye Serikali imesikia kilio chao na kupeleka mashine hiyo ya kisasa kama ilivyoahidi.

Akiendelea na ziara ya kutembelea hospitali ya Rufaa ya Morogoro na vituo vya afya katika manispaa ya Morogoro leo Alhamis Januari 16,2020, Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe. Abdulaziz Abood (CCM) amejionea mashine hiyo ikifanya kazi.

Mhe. Abood ameishukuru serikali kwa kutekeleza ahadi yake hiyo na kuwajali wananchi wa mkoa wa Morogoro kwa kuleta mashine ya kisasa kwa ajili ya huduma za X-ray kwani kilikuwa ni kilio cha muda mrefu ambacho amekuwa akiiomba Serikali kuwasaidia kifaa hicho.

Mhe. Abood amesema mara kadhaa amekuwa akiomba kupatiwa mashine hiyo hata akiwa bungeni na amemshukuru Rais Magufuli kwa kusikiliza ombi hilo maalum na kuwapatia mashine hiyo ya X-ray ya kisasa.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro,Dkt.Ritha Lyamuya amesema mashine hiyo imekuwa msaada mkubwa kwao kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kazi hali ambayo amesema imesaidia hata kupunguza malalamiko ya wagonjwa ambao walikuwa wakikosa huduma ya X-ray kutokana na mashine iliyokuwepo awali kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi.

Dkt. Lyamuya amesema mashine hiyo ina uwezo mkubwa wa kufanya kazi na hivyo kusaidia hata kupunguza idadi ya wagonjwa ambao walikuwa wakipewa rufaa kwenda hospitali ya taifa muhimbili kwani mashine hiyo ina uwezo wa kutuma taarifa za mgonjwa kwa njia ya mtandao na kurejesha majibu ndani ya muda mfupi.

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe. Abdulaziz Abood (katikati) akipokea maelezo namna mashine ya X-ray ya kisasa inavyofanya kazi katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe. Abdulaziz Abood (katikati) akipokea maelezo namna mashine ya X-ray ya kisasa inavyofanya kazi katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.

December 01, 2019

Image result for twaha kiduku na dullah mbabe" 
Baada ya Bondia Twaha Kiduku wa Morogoro kutangaza hadharani akitaka mpambano na Bondia kutoka Dar Es Salaam Dulla Mbabe, sasa ni rasmi. Promota Ally Mwanzoa wa Tanga, ametaka mabondia hao kukutana naye na kuandaa pambano kati yao. Promota Mwanzoa amewapa Uhuru mabondia hao kuipanga tarehe na mwezi watakaotaka kupigana ila waende mezani wakaini mikataba ya pambano hilo.


 
Bondia Twaha Kiduku alipokewa kishujaa Mkoani Morogor, kufuatia mapokezi aliyoandaliwa wakati akireje mkaoni hapa baada ya kumtwangwa vilivyo bondia kutoka Afrika Kusini France Thabang Ramabolu katika pambano la utangulizi la mchuano uliowakutanisha Hassan Mwakinyo kutoka Tanzania na Arnel Tinampay kutokea Philipino mpambano ambao ulimalizka kwa Hassan Mwakinyo kuibuka mbabe kwa Point.
Twaha aliwasili Morogoro mida ya saa nane mchana na kupokewa na mamia ya wakazi wa Mji wa Morogoro na kusababisha baadhi ya shughuli kusimama kwa muda. Akizungumza nasi katika mapokezi hayo, mratibu wa mapokezi hayo Jackson Jackson Charles Busanda amesema amefurahishwa na muitikio mkubwa wa wakazi wa Morogoro licha ya kuandaa tukio kwa muda mfupi. Naye kwa upande wake Bondia Twaha amewashukuru wakazi wa Morogoro kwa mapokezi yale na kusema hana cha kuwalipa zaidi ya kuwawakirisha vema katika mashindano mengine. #hongera sana Twaha Kiduku


November 24, 2019

Image may contain: 1 person, smiling, standing and text
Ni wimbo wa kwanza wa Birthday kwa upande wa muziki wa Singeli. Wimbo huu umetolewa maalum kabisa kwa mtangazaji mahili mkoani Morogoro toka Planet Fm Bibie Warda Makongwa, aliyeadhimisha kumbukumbu yake ya kuzaliwa Siku ya jana katika ukumbi wa BZ Hotel. pia wimbo huu sasa ni rasmi kwa ajili ya Birhday Yako ama mshkaji wako.


DOWLOAD HAPA

Official Video ya mwanamuziki mkali wa Free Style kutokea mkoani Morogoro Rajram   
(RAJRHYMES )  imekamilika na nipo hewani nkwa ajili yako shabiki na mdau wake .

      

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE