![]() |
Berry Black akipagawisha jukwaani |
NYOTA wa muziki wa kizazi kipya Mbaraka Abdallah anatarajia kutambulisha wimbo wake mpya uitwao Nyumbani Sio Safi, Jumapili kwenye Ukumbi wa Club Billicanas.
Berry amesema katika onyesho hilo maalumu kwa ajili ya utambulisho wa wimbo wake, ataambatana na msanii mwenzake Isihaq Salehe ‘Easy Man’, anayeng’ara na kibao cha Kasoro Wewe.
“Katika onyesho hilo la Jumapili nitatambulisha wimbo wangu huo lakini pia nitakuwa na nyingine kibao za kuwapagawisha mashabiki wangu, nikisindikizwa na swahiba wangu Easy Man,” alsiema Berry Black.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment