May 22, 2012

Jana ilikuwa siku ya kumbukumbu ya miaka 16 tangu kutokea kwa  ajali ya MV Bukoba.Kumbukumbu ya ajali hiyo iliyosababisha vifo kwa maelfu ya watanzania ilifanyikia huko mkoani Mwanza.
Pamoja na matukio mengine kadhaa ya kuadhimisha kumbukumbu hiyo, Mtanzania mwenzetu,mwanamitindo Flaviana Matata, yeye alichukua hatua moja zaidi. Anataka kuhakikisha,kwa vitendo, kwamba hata kama ajali ya namna ile ambayo ilichukua maisha ya mama yake mzazi itatokea tena,basi uwepo uwezekano mkubwa wa maisha ya watu kutopotoea.
Kupitia taasisi anayoiongoza ya Flaviana Matata Foundation(FMF), na akisindikizwa na washirika wake wa karibu kama vile Maria Sarungi,Shamim Mwasha na wengineo, alitoa Life Jackets 500 ambazo alimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Elias Makori, ili zitumike katika shughuli za usafiri wa majini hususani katika Ziwa Victoria.
BC inapenda kuendelea kumpa pole Flaviana kwa kuondokewa na Mama yake mzazi kupitia ajali ile mbaya ambayo bado inaaminika kuwa mbaya kupita ajali zote za majini nchini Tanzania. Lakini pia tunapenda kukupa pongezi kwa hatua aliyochukua ya kuhakikisha kwamba maisha ya wengine hayapotei.Ni mfano wa kuigwa.Pongezi nyingi zikufikie Flaviana.
Hizi hapa ni baadhi ya picha kutoka katika tukio hilo. Picha zote kwa hisani ya Shamim Mwasha(8020 Fashions)
Flaviana Matata akikabidhi msaada wa maboya 500 kwa mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Mwanza, Elias Makori kulia ikiwa ni kumbukumbu ya miaka 16 ya ajari ya meli ya MV Bukoba, anayeshuhudia ni Meneja Masoko na Biashara wa Shirika la usafirishaji wa majini mkoani Mwanza la Marine Service,Kapten Obadia Nkongoki. Igoma jijini Mwanza,
Flaviana akionyesha moja ya maboya yenye nembo ya foundation yake aliyokabidhi katika kumbukumbu ya miaka 16 ya ajali ya MV Bukoba ikiwa ni kampeni yake ya kupunguza ajari za majini hapa nchini.
Flaviana Matata akishindwa kujizuia na kuangua kilio wakati wa ibaada ya kumbukumbu ya miaka 16 ya ajari ya meli ya MV Bukoba alipotembelea baadhi ya makaburi ya watu waliopoteza maisha katika ajari hiyo yaliyopi Igoma jijini Mwanza, katika ajali hiyo Flaviana alimpoteza pia mama yake mzazi.
Flaviana na wageni wakiweka  mashada kwenye makaburi ya waliofariki kwenye ajali hiyo Igoma Mwanza

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE