Akiongea na mwandishi wetu kwa njia ya simu, msemaji wa kundi hilo, Nick Simon...alisema albam hiyo itakuwa na nyimbo 20, ambapo imehusisha nyimbo za wasanii kama Joh Makini, Lord Eyes, Bonta, Nick na Gnako.
“Albamu ipo katika hatua za mwisho na tumeifanya katika studio tofauti ili kuleta mchanganyiko wa ladha, tunakusudia kuisambaza wenyewe kupitia mawakala wetu waliopo Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na mikoa mingine ili kuepukana na ulanguzi uliopo sasa,” alisema.
Wasanii walioshirikishwa katika albamu hiyo ni Juma Nature, Peter Msechu, Belle 9, Pipi na Fundi Samweli.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment