August 18, 2012

Diamond  na  Dimpoz   wwakirishi  wa  Kigoma  All  star


Habari za kuamika kutoka kwa vyanzo mbalimbali zinadai kuwa wasanii wa mkoa wa Tanga wamelikataa wazo la mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe la kufanya wimbo wa pamoja kama Tanga All Stars kwa madai kuwa mradi huo anaufanya ili kujinufaisha kisiasa.

Hivi karibuni Mheshimiwa Zitto alikiri kuutaka urais wa Tanzania wakati wa mahojiano na kipindi cha Makutano cha Magic FM na watu wengi wamekichukulia kitendo cha kuwa karibu na wasanii wa Tanzania kama njia ya ya kujiimarisha kisiasa na kuwashawishi vijana walio wengi nchini.

katika  mazungumzo ya  simu   na MwanaFA  jana (August 17) ambaye amesema wasanii wa Tanga wana program yao wenyewe iliyopo tangu muda mrefu na wamewahi hata kufanya show za ndani na nje.





Mwana  FA- Toka  Tanga


Amesema hawawezi kujiingiza kwenye mradi huo wa Zitto kwakuwa umekaa kisiasa zaidi.

Katika mahojiano na kipindi cha XXL cha Clouds FM mwezi uliopita, Zitto alidai kuwa lengo lake ni kila mkoa kuwa na wimbo wa nyota wenye asili ya mikoa mbalimbali na baada ya Kigoma mkoa wa pili aliokuwa anafanya nao mazungumzo ni Tanga ambao tayari wamemtosa.

Wakati Tanga ikishtukia mchezo huo wenye harufu ya siasa, wasanii wa Morogoro chini ya Afande Sele tayari wameingia mkenge na wamefanya wimbo wa Morogoro All Stars.

Morogoro All Stars inaundwa na Afande Sele, Koba, Stamina, Belle9, Samir, Criss Wamaria, Nassa, Oten, Dayna na Zilla!





.   Afande   Sele-  mwakilishi  wa  MORO  ALL  STAR

Chanzo kimoja cha uhakika kimethibitisha kuwa mradi wa Kigoma All Stars umegharimu mamilioni ya shilingi.

Amedai kuwa kwenye show ya wasanii hao iliyofanyika mwezi uliopita mkoani Kigoma kila msanii alilipwa si chini ya shilingi milioni moja.

Aidha Mheshimiwa Zitto aliwahi kudai kuwa Kigoma All Stars itakuwa kampuni na inajenga kituo cha kuendelea vijana wenye vipaji mbalimbali mkoani Kigoma.





   MBUNGE Zitto  Kabwe -Msimamizi  wa  KIGOMA  ALL STAR


Kufuatia wasanii wa Morogoro kuja na wimbo wao kama wale wa Kigoma, kumekuwepo na hisia tofauti juu ya miradi hiyo ya wasanii kujiunga na kutoa nyimbo za mikoa ambapo wapo wanaosema ni kitu kizuri huku wengi wakidai inaonesha jinsi watu walivyoishiwa na mawazo mapya.
“Uvivu wa fikra na maisha ya kuiga...wangeweza kufanya kitu nyingine nzuri ya kibunifu kuliko ku-kopi na ku-paste...upu********....kila kukicha tunalala na kuamka kushughulika idea ambayo tayari wenzetu washachomoka nayo..lets not waste time on the same thing always while we can think in wide angle and come up with mo amazing things in the Industry...ghosh....!!!,” alisema mchangiaji aitwaye 
 Likati.

‘Nyerere alikatataa makundi ya ukanda na ukabila nini sasa hii? mimi ni mdau wa burudani Tanzania, hii kitu naona haina maana kabisa zaidi inakuja haribu 

Habari  ni  kwa  hissani  ya   Leotainment


Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE