
Akiongea na U Heard ya Clouds FM leo, mume huyo aliyejitaja kwa jina la Jose mkazi wa Kasulu mkoani Kigoma amesema mke wake aitwaye Salma amejifungua mtoto anayefanana kila kitu na Chege.
Akizungumza kwa jazba, Jose amesema yuko tayari kwenda kuchukua vipimo vya DNA na kama vikionekana negative atamlipa Chege shilingi milioni tano.
Amesema kesho anaanza safari yake ya kuja Dar es Salaam kumleta Salma na mwanae kwa Chege ambaye anasema ndiye baba yake mzazi huku akitishia kumfanyiaa kitu mbaya staa huyo.
Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Chege aliyekuwa akiongea kwa dharau amesema hajui lolote na wala hamfahamu Salma.
Kwa upande mwingine wadau wemesema kwamba inawezekana ni story ya uwongo CHEGE labda ametengeneza kwani wasanii wengi sasa hivi huwa wanajitungia skendo ili wapate kuzungumzwa hasa wanapiokuwa na nyimbo mpya au wanapokaribia kutoa nyimbo mpya.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment