Jan usiku zilitapakaa habari kuhusu kifo cha msanii wa BONGO Freva na tasnia ya Filamu maarufu kwa jina la Sharo Milionea
Kufikia majira ya saa tano kasoro usiku Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga alitibisha taarifa hizo kupita kipindi cha ALA ZA ROHO kinachorushwa na kituo cha Clouds fm chini ya mwana dada DIVA. Kamanda kizungumza na Suody Brown alisema
'' “leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza” Kamanda amesema hakuna kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo gari imehifadhiwa mahali salama kwa sababu haitembei. Kwenye gari alikua mwenyewe''
Tumeshindwa kuweka picha za mwili wa Marehemu kutokana na sababu muhimu za kibin adam. Samahini kwa ilo.

0 MAONI YAKO:
Post a Comment