Watu wanne wamekamatwa na Jeshi la Police kwa tuhuma za
na kumuibia marehemu Sharo Milionea baada ya kupata ajali ya
gari na kupoteza maisha.
Kwa mujibu wa website ya thisisdiamond.com watu hao
wamekutwa na vitu alivyokuwa navyo marehemu Sharo Milionea kama vile
T-shirt,
Viatu, Simu ya mkononi, Pete, Cheni, Tairi moja la gari , pamoja na Battery la
gari ambalo marehemu alipata nalo ajali.
Taarifa za awali zinasema watuhumiwa hao walikuwa sita
lakini wamekamatwa wanne hadi sasa, na jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka
watuhumiwa wawili.
Inasemekana watu hao waliamua kumkata vidole marehemu baada
ya kushindwa kumvua pete.
Hata hivyo jeshi la polisi bado halijatoa taarifa rasmi
kuhusiana na kukamatwa kwa watu hao.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment