
Yakiwa yamebakia masaa machache ili mkali wa hip hop toka mjini Morogoro, Stamina Kabwela Supermario ili aachie wimbo wake mpya aliomshirikisha mkali wa hip hop toka Mwanza Fid Q ngosha uitwao wazo la leo, mkali huyo amefunguka na kawomba wadau wampe sapot kwa kununua wimbo huwo kwa silingi elfu tatu TSH: 3000/= kama alifyofanya R.O.M.A kwa wimbo wake.
Akizungumza na ubalozinirespect.blogspot,com leo mchana, Stamina amesema
'' Ebwana wimbo wangu mpya nimeamua kuwapatia kwa Tsh: 3000/= na nnawaomba ndugu zangu wanisapot kwa hilo, mziki ni maisha, mziki ni kazi kama kazi zingine, kwa hiyo ili uweze kuupata wimbo wangu utalipia kiasi icho cha pesa kwa maana ya kunisapot ili nami nipate moyo wa kufanya kazi nzuri zaidi, kwa wewe unayempenda Stamina, unayependa mziki wa bongo na unayehitaji mafanikio ya wanamuziki wako basi huna budi kusapoti hilo. Elfu tatu ni kubwa lakini kutokana na maisha ya sasa imebidi iwe hvyo'' .Amesema Stamina

Stamina moja ya matamasha aliyofanya
Pia amesema kesho ikiwa ndiyo siku mzigo unakuwa mtaani atatoa utaratibu wa kuweza kununua wimbo huwo na wewe jinsi ya kuweza kuupata.
Maoni ya blog hii: ifikie hatua tubadilike, tuwe na moyo wa kweli wa kusapot mziki na wanamuziki wetu kwa kununua nyimbo zao na kuingia ktk show zao ili wapate moyo zaidi wa kufanya vizuri
0 MAONI YAKO:
Post a Comment