
Msanii wa muziki wa Hip Hop toka mkoani Morogoro mwenye taji la ufalme, afande Sele amesema lengo la kuandika wimbo wa Dini Tumeletewa ni kutaka kumrudisha mwafrika katika tamaduni zake. Katika ukurasa wake wa Facebook Afande amepost. Katika wimbo huwo ambao Mbunge wa Kigoma Kaskazini Kabwe Zuberi Zitto amehaidi kuufanyia Video kwa pesa yake, Afande amejaribu kuzungumzia amani, imani na mila kuhusiana na kuabudu.
''Lengo la hii kazi yangu mpya DINI TUMELETEWA ni kumrudisha mwafrika kwenye uafrika wake ambao msingi wake ni UMOJA, USHIRIKIANO NA UPENDO. Ambao kwa siku za hivi karibuni tumeshuhudia ukitoweka. Tumeona mapigano/mauaji ya itikadi za kidini wenyewe kwa wenyewe, pia kuelezea uhuru wa kuabudu kwa imani yoyote bila kuvunja sheria za Taifa letu. Kwa mtu yoyote makini mwenye mapenzi mema kwa Taifa letu na AFRIKA hawezi kupingana na hilo, kwa kutambua hilo MH; ZITTO ZUBERI KABWE(ZZK) kajitolea kugharamia gharama zote kwa ajili ya kufanikisha vidio bora kabisa ya wimbo huu, hii ni kazi yetu wote mimi na wewe, tunasema asante sana kwa Mh; Zitto. AMANI NA UPENDO KWANZA''
0 MAONI YAKO:
Post a Comment