August 20, 2013

WANAMUZIKI wawili wenye majina ya kutisha, Waziri Sonyo na Rais wa zamani wa bendi ya Victoria Sound, wamepigana katika mazoezi ya bendi yao yaliyofanyika Mbagala, jijini Dar es Salaam

  Waziri Sonyo kushoto.

Katika kichapo hicho, inadaiwa kuwa Sonyo nusura amchome Muumini kisu, hivyo kuzua hofu katika patashika ya aina yake inayoendelea kuonyesha mgogoro mkubwa kati ya wanamuziki hao ndani ya Victoria Sound.

Akizungumza muda mchache baada ya kadhia hiyo, Muumini alisema alishangaa kujikuta yupo chini na Sonyo akiwa ameshatoa kisu kutaka kumjeruhi.
Muda mchache baadaye Muumini aliandika kwenye mtandao wa kijamii akielezea tukio hilo alilodai ni la aina yake huku akitumia lugha kali za kuudhi dhidi ya Sonyo.

“Leo ndio nimedhihirisha huyu ( hapa kuna tusi ila limefichwa kwa sababu za kiungwana) ni kweli yy amenikuta nimekaa tena pembeni na tahadhali zote ila alivyokuja kwangu kunivamia sikumkawiza nikampa ngumi 3 takatifu zilizolenga uso wake ndio akaona kumbe huyu mzima akatoa kisu mfuko wa kulia watu ndio wakamshika lakini wakati nakwepa kisu nilianguka kama sio George Gama ameshanijeruhi au kuniua kabisa ngoja nimfunze adabu nampeleka mahakamani ili iwe fundisho na kwa ili sina msalie mtume hivi jimwili lote la Sonyo Bado anamshikia mwanaume mwenzie Kisu na amshukuru Janurry aliyenipakata ningempukutisha meno kwa ngumi maana alikuwa kama kuku mgonjwa hakurusha hata ngumi," mwisho wa kuipitia meseji ya Muumini.

Kupigana kwa wanamuziki hao ni mwendelezo wa mgogoro mzito uliokuwapo kwa bendi hiyo baada ya uongozi pia kumuondoa katika nafasi ya urais Muumini na kumpa Kassim Muhumba, huku pia Sonyo akienguliwa katika nafasi yake ya kiongozi wa shoo
Katika kichapo hicho, inadaiwa kuwa Sonyo nusura amchome Muumini kisu, hivyo kuzua hofu katika patashika ya aina yake inayoendelea kuonyesha mgogoro mkubwa kati ya wanamuziki hao ndani ya Victoria Sound.

Akizungumza muda mchache baada ya kadhia hiyo, Muumini alisema alishangaa kujikuta yupo chini na Sonyo akiwa ameshatoa kisu kutaka kumjeruhi.
Muda mchache baadaye Muumini aliandika kwenye mtandao wa kijamii akielezea tukio hilo alilodai ni la aina yake huku akitumia lugha kali za kuudhi dhidi ya Sonyo.

Related Posts:

  • Liberia imefanikiwa kutokomeza Ebola-WHOImage copyrightGettyImage captionMtu aliyenusurika ebola Shirika la afya duniani WHO, limetangaza kwua taifa la Liberia, limefanikiwa kutokomeza Ugonjwa wa Ebola kwa mara ya pili. Mei mwaka huu shirika hilo lilikuwa limetoa t… Read More
  • Mashekh waliotekwa, waachiwa huruKatibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya kuachiwa huru kwa Mashekhe waliotekwa nchini DRC. Kushoto ni Mkurug… Read More
  • Magazetini Leo Kutoka Dar es Salaam Tanzania leo Ijumaa Septemba 4,2015 tumeingia kwenye chumba cha cha TZA kinachomiliikiwa na Millard Ayo na tayari tumeyakusanya Magazeti yote na stori zake kubwakubwa kukusogezea hapa, headlines baa… Read More
  • Mgombea mwenza wa UKAWA Juma Haji Duni atikisa jimboni kwa Nape Wafuasi wa Ukawa wakishangilia.   Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji...  Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akisalimiana na mfuasi wa Ukawa wakati alipowasili katika mkutan… Read More
  • Lowassa awasili Mpanda kwa Chopa Chopa iliyowabeba Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mwenyekiti wake, Mh. Freeman Mbowe, ikitua kwenye … Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE