October 14, 2013

 

  Katika kuadhimisha miaka kumi na nne tangu Rais wa kwanza wa Tanzania   Mwl J. K. Nyere  kufariki, watanzania wamezidi kumkumbuka kwa mambo yake na uongozi. Mwl atakumbukwa kwa mengi juu ya Taifa ili.
  Baadhi ya Watanzania waliotoa mitazamo yao juu ya Mwlm kupitia sehemu mbalimbali ni pamoja na wasanii, wadau na watanzania kwa jumla. Dayna Nynge alikuwa ni msanii wa kwanza kutoa yake kupitia Page yake ya Facebook, akiungana na wadau wengine.



Photo 
DAYNA
Ni miaka kumi na nne sasa tangu ulipotutoka, ilikuwa th 14 oct 1999 alhamisi kilitangazwa kifo chako.
Nchi ilipata pigo, tukifikilia mengi juu ya harakati zako na nchi hii. Ulikuwa mstari wa mbele katika kutetea misingi ya haki, amani, mshikamano na umoja, tulilia kufikilia pengo lako tukisema halitazibika. Ukweli ni huu mpaka leo hii pengo lako lipo. Migongano ya kisiasa, purukushani bungeni, bunge limekuwa kijiwe cha vijembe na kashfa ,hekima zako hazipo, matukio ya kiharifu kila kukicha. Tukuombe uliombee taifa hili huko ulipo, tunakuombea kwa allah akusamehe ulipokosea kwani wewe ni binaadamu, tunakukumnuka, tulikuhitaji, bado tunakuthamini Mwl J K Nyerere. Pumzuka pema peponi
Unlike · ·

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE