Mkurugenzi wa Katiba,Sheria na Haki za Binadamu wa NCCR-Mageuzi, Dk
Sengodo Mvungi amefariki dunia leo alasiri nchini Afrika Kusini
alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa na watu 9 wanaosadikiwa
ni majambazi.
Dk Mvungi ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
alijeruhiwa kwa kukatwa na mapanga kichwani Novemba 13, mwaka huu
nyumbani kwake Kibamba Msakuzi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na
kulazwa Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (Moi) na baadaye kuhamishiwa
Hospitali ya Milpark, Johannesbarg, Afrika Kusini.
Oh my God, this is bad, bad , bad news
ReplyDelete