Mabaunsa wakimkinga Liyumba.
ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Miradi wa Benki
Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba, leo alitinga katika mahakama ya
Kisutu kusikiliza kesi yake akiwa na kundi la mabaunsa waliokuwa
wakimkinga asipigwe picha na mapaparazi. Liyumba alitinga mahakamani
hapo kusikiliza kesi inayomkabili ya kunaswa na simu ya kiganjani akiwa
gerezani ambapo leo ilikuwa siku ya kumsikiliza shahidi wa upande wa
mashitaka lakini shahidi huyo alipatwa na udhuru hivyo kesi hiyo
kuahirishwa mpaka Novemba 26 mwaka huu.
PICHA : RICHARD BUKOS / GPL
0 MAONI YAKO:
Post a Comment