November 23, 2013

                         
Ile ndoa iliyofungwa kwa mbwembwe na kufuatiwa na tafrija kubwa kati ya wasanii wa filamu za Kibongo, Salome Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ na Mike Sangu imevunjika rasmi baada ya mizozo ya mara kwa mara.

Chanzo makini cha kuaminika kilichopo karibu na wanandoa hao kimesema ndoa hiyo ilivunjika rasmi Oktoba mwaka huu na sababu kubwa ikiwa ni kupigana mara kwa mara. “Unajua nyie mliandika ndoa imevurugika na Thea ameenda kwao eti atarudi watakapokaa na kuyazungumza, mmefichwa, Mike na
Thea wameshaachana na hakuna anayemhitaji mwenzake tena na Thea ameondoka na vyombo vyake vyote,” kilisema chanzo hicho.

Inadaiwa kwamba hata katika msiba wa dada yake Mike uliotokea hivi karibuni, Thea ingawa alikuwepo, lakini hakujishughulisha na lolote wala sare ya msiba hakuvaa na aliyeonekana kuchukua majukumu yake ni mke wa zamani wa Mike aitwaye Kuruthum Mpalu ‘Ummy’.

“Siku hiyo kila kitu kilikuwa wazi, mlishindwaje kubaini? Thea hakuwa karibu kabisa na alikuwa na mawazo tele, Ummy ndiye alikuwa ‘mother house’ na wengine wanadai amerudiana rasmi na Mike,” kiliendelea kutoboa chanzo hicho.

Kufuatia nyeti hizo, waandishi wetu walimsaka Thea na kufanikiwa kumpata bila hiyana akaweka mambo hadharani.
“Mh mnatafuta umbeya tu hapa, mimi nimeachana na Mike mbona siku nyingi tu, nyinyi ndiyo mnajua leo?” aliuliza.
Katika hilo, Thea alisema ana sababu nyingi zilizomfanya kuachana na Mike na kwamba baadhi yake hawezi kuziweka hadharani, lakini kubwa ni vipigo vya mara kwa mara kutoka kwa mwanaume huyo, kiasi kwamba ameshindwa kuvumilia kutokana na hasira alizonazo.

Thea alisema baada ya kuachana na Mike, ameamua kupumzika mambo ya wanaume kwa miaka miwili kabla ya kuamua vinginevyo maana ndoa hiyo imemchosha.
“Siwezi kusema sitaolewa tena, ila napumzika na ikitokea kuolewa itakuwa ni baadaye sana lakini katu sitarudi kwa Mike labda Yesu arudi,” alimalizia Thea.

Kwa upande wake, Mike alipopigiwa simu na kuulizwa kuhusu ndoa yake na Thea alikiri kuwepo kwa jambo hilo, akisema haelewi hasa kisa ni nini, lakini anaamini atajua baada ya muda siyo mrefu.

“Thea ameondoka kweli. Kuhusu siku ya msiba wa dada ni kweli Ummy alikuja na kunisaidia, lakini siyo kama tumerudiana isipokuwa yule ni mzazi mwenzangu na alijua kwamba Thea hayupo, ni hivyo.”

Related Posts:

  • Tazama show ya Jagwa Musi Band   Ni kundi la muziki asili wa Mchiriku toka nchini Tanzania. Ni miungoni mwa makundi machache sana yanayofanya mziki huo wa Mchiriku. Mziki wa Mchiriku ni mziki uliopata umaarufu sana mwanzoni mwa miaka ya 90 mpaka… Read More
  • Video: Chindo Man ft Wakazi,Fid Q & Dully Sykes – Torati ya Mtaa Ki ukweli kabisa, ukizungumzia makundi ya mziki wa Hip Hop hapa Tanzania lazima hutaacha kulitaja hili kundi la Hip Hop toka Jijini Arusha linaloitwa Watengwa. Sasa hii leo mtengwa Chindo Man ametuletea wimbo wake unaitw… Read More
  • RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ) - Sehemu ya Tisa Mtunzi: Enea Faidy Ilipoishia Sehemu ya 8 ( Bofya hapa Kama Hukuisoma ) ..Mwalimu John alipelekwa makuburini kwaajili ya mazishi ingawa yeye alijiona yuko hai. Dorice alikuwa njiani baada ya kutoroka shulen,… Read More
  • Brand New Audio: Mash J ft G-Nako- Taarifa Mkali wa Hip Hop toka mkoani Morogoro Mash J Mperampera ameachia Audio ya wimbo wake wa Taarifa aliomshirikisha G-Nako. Wimbo huo uliofanywa na Producer Vennt Skillz wa Kwanza Record za Mkoani Morogoro Video yake ilian… Read More
  • Move ya kukumbukwa  Kariobu mpenzi msomaji wa ubalozini.blogspot.com. Leo ikiwa ni siku ya jumapili, tumekuwekea move ya Wrong Turn 3: Left for Dead iliyotoka mwaka 2009. Malizia wikend yako kwa kutazama Move hii yua kukumbukwa &nbs… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE