December 27, 2013

Mtoto wa Kiume, Geez Mabovu ameamua kufanya mabadiliko katika maisha yake pale tu kalenda itakapobadilika na kuonesha mwaka tuliopo ni 2014.
Mabovu ambaye amesherehekea siku yake ya kuzaliwa  wakati dunia ikisherehekea sikukuu ya Christmas (December 25), ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa amepanga kufanya mabadilko makubwa katika maisha yake ikiwa ni pamoja na kuacha rasmi kunywa pombe kuanzia January Mosi.
“Kitu ambacho nataka kubadilisha katika maisha haya ya sasa hivi ni kuacha pombe tu, niache kunywa pombe tu basi. From January 1, ntastart hivyo yani. Sikupromise lakini ntafanya hivyo, kwa sababu ni mimi na maamuzi yangu binafsi.” Mabovu ameiambia tovuti ya Times Fm.
Mabovu amesema amechukua uamuzi huo kwa sababu anaamini hakuna kitu chenye mwanzo kinachokosa kuwa na mwisho na kwamba maamuzi ni ya mtu mwenyewe.
Rapper huyo amefunguka kuwa kwa watu ambao wanamfahamu na walikaa nae siku zote wanafahamu aliacha kuvuta marijuana miaka tisa iliyopita.
“Kwa ambaye amewahi kukaa na mimi jirani kwa wiki moja ama wiki mbili tukawa tuko pamoja, mi bangi niliacha miaka tisa iliyopita. Kwa hiyo sijavuta bangi miaka tisa, nikabaki kwenye pombe na ndio naendelea kujirekebisha.” Ameeleza Geez Mabovu.
“Kwa hiyo hao watakaokuwa wanaongea, wataongea kwa sababu mimi ni flani. Wao kivyao hawawezi  kuzungumzia maisha yao binafsi, na wananizungumzia kwa sababu…hamna sababu ambayo mtu mwingine anaweza kukuzungumzia eti akamzungumzia mtu mwingine ambaye hajulikani duniani.” Mtoto wa Doll South amefunguka.
Hivi karibuni Geez ameachia wimbo mpya aliwashirikisha Profesa Jay na AY,wimbo unaitwa Hapa Kule.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE