December 18, 2013

Jaguar anunua gari ya shilingi milioni 288 za Tanzania               
Msanii wa Kigeugeu, Jaguar ameongeza ndinga ya gharama kwenye orodha ndefu ya magari yake ya bei mbaya.
 Msanii huyo wa Kenya aliionesha gari yake mpya kwenye concert ya miaka 50 ya uhuru wa Kenya kwenye uwanja wa Kasarani jijini Nairobi Ijumaa iliyopita.
 Gari hilo aina ya Jaguar ni la rangi ya kijivu na lina thamani ya shilingi milioni 16.8 za Kenya ambazo ni sawa na shilingi milioni 288 za Tanzania.
Kwa mujibu wake mwenyewe, gari hilo halipitishi risasi na limetengenezwa kwaajili yake (custom-made).

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE