December 10, 2013


 Wachezaji wa mpira wa miguu wa Ivory Coast, Didier Drogba na Emmanuel Eboue watawajibishwa na kamati ya nidhamu ya chama cha mpira wa miguu cha Uturuki, baada ya kuonesha uwanjani flana zenye maandishi yanayoonesha heshima kwa Nelson Mandela.
Baada ya Galatasaray kupata ushindi Ijumaa iliyopita, Drogba alionesha flana iliyoandikwa ‘Thank you Madiba’, wakati Eboue alionesha flana iliyoandikwa ‘Rest in peace, Nelson Mandela’.
Kwa  mujibu wa sheria za chama cha mpira wa miguu cha Uturuki, mchezaji haruhusiwi kuonesha flana zenye ujumbe wa aina yeyote bila kupewa ruhusa maalum na chama hicho.
Hata hivyo pamoja na kukabiliwa na tishio hilo la kulipishwa faini, Drogba alipost kwenye Instagram picha inayoonesha akiwa uwanjani na flana yenye maandishi ‘Thank you Madiba’, na kuandika ‘Thank you for everything’

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE