Kwa mujibu wa kalenda hiyo, wanaanza ‘Year of the Horse’.
China inaukaribisha mwaka mpya kwa mujibu wa kalenda yao inayofuata mbalamwezi ‘Lunar Calendar’, na watasherehekea kwa takribani siku kumi na tano (hadi February 15).
Kila siku ya sherehe hizo katika siku hizo kumi na tano inakuwa na ishara ama maana maalum kwa mujibu wa tamaduni za Kichina. Kwa mfano, siku ya tisa ni siku watakayoadhimisha kuzaliwa kwa mfalme wa mbingu, Jade Emperor, na Mungu wa utajiri/mali anaaminika kumwaga baraka zake katika siku ya tano ya sherehe hizo.
Watu mbalimbali kutoka nchi za jirani wameanza kuingia China kushuhudia sherehe hizo zinazoambatana na maonesho ya tamaduni za kichina, huku mapambo ya farasi na dragon yenye rangi nyekundu yakiwa yanatawala katika maeneo mbalimbali
0 MAONI YAKO:
Post a Comment