Mh: Edward Ngoyai Lowasa
Waizri mstaafu, Edward
Lowassa, LEO ametangaza kuanza safari ya matumani ya ndoto zake ambayo
itawasaidia Watanzania kupata elimu bure, maji safi na maendeleo ya
uhakika na pia amesema anapowatazama marafiki zakengu machozi
yananitoka.
Lowassa ametoa kauli hiyo LEO katika ibada ya shukrani na kuupokea mwaka mpya iliofanyika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Monduli mjini.
Lowassa wakati akitoa kauli hiyo hakutaja safari hiyo ni ipi Zaidi aliwashukuru watu wote ambao walimsindikiza kwenye ibada hiyo.
Lowassa amesema anaamini watu wana uhakika wa ushindi katika safari hiyo kwa kumtegemea mungu.
“Nimefarijika sana LEO kuwaona hapa marafiki zangu wengi, ninapowatazama hadi machozi yananitoka na kwa uwezo wa Mungu tutashinda kwani nyote mnajua nia na ndoto yangu,’’amesema Lowassa na kupokelewa na sauti za shangwe kanisani.
KATIBA MPYA
Lowassa amesema licha ya kumpongeza Jaji Joseph Warioba kwa maelezo yake kuhusu muundo wa Serikali tatu, anawasiwasi na muundo huo.
“Mimi nawasiwasi na huu muundo ni vyema viongozi wa dini, kuliombea taifa tupate katiba bora kwani maoni ya watu 40 asilimia ambao hawakutaka muundo wa serikali tatu lazima yatazamwe,”amesema Lowassa
0 MAONI YAKO:
Post a Comment