Mbwana Samata, mshambuliaji anaeichezea klabu ya TP Mazembe,
amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka 2013 wa klabu hiyo ya TP
Mazembe.
Mbwana alipata kura nyingi zaidi, kuwashinda wenzake, ambao kwa
mujibu wa tovuti ya TP Mazembe, yeye alipata pointi 248, huku nafasi ya
pili ikishikwa na Asante Solomon aliepata kura 219.
Ulikuwa ni mwaka wa mafanikio pia kwake, pia akiwa na kumbukumbu ya
kutajwa kati ya wachezaji ambao wanawania tuzo za Wachezaji wanaocheza
barani Afrika, nakuchujwa baadae.
Zaidi ya hiyo, ameisaidia timu yake ya TP Mazembe katika michuano ya
ndani na kimataifa, bila kusahau msaada pia aliuutoa kwa timu yake ya
Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment