January 21, 2014


  Aliyekuwa muigizaji maarufu wa Isidingo Lesego Motsepe aka Lettie, amekutwa akiwa amefariki Jumatatu (January 20),  nyumbani kwake Johannesburg, Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa mtandao wa drum, kaka yake anayejulikana kwa jina la Moemise Motsepe alikuwa mtu wa kwanza kufahamu kuhusu kifo chake baada ya kuukuta mwili wake nyumbani kwake majira ya saa tano asubuhi, lakini kifo chake kilithibishwa rasmi majira ya saa saba mchana, ambapo ilielezwa kuwa kilisababishwa na sababu asilia (natural causes).
Lesego alikuwa anaishi na virusi vya ukimwi na alijitangaza rasmi katika siku ya Ukimwi duniani (December 1, 2011) na kudai kuwa alikuwa akiishi na virusi hivyo tangu mwaka 1998.
Tangu alipojitangaza hadharani, alitumia nafasi yake kama muigizaji maarufu katika kuhakikisha anasambaza elimu kuhusu jinsi ya kujikinga na virusi vya ukimwi, na jinsi ya kuishi kwa matumaini kwa wale walioathirika. Na kwa muda wa miaka zaidi ya kumi amefanya kazi hiyo akiwa kama balozi (Aids ambassador).
Kufuatia kifo hicho, familia yake imetoa ombi kwa wale wote wanaotaka kumuenzi waige mfano wake wa huduma aliyojitolea kwa jamii.
“Honor her example of service, accomplishment and modesty, and the next time you walk outside on a clear night and see the moon smiling down at you, think of Lesego Motsepe and give her a wink while speaking words of courage declaring life to lifeless situations.” Alisema msemaji wa familia ya Lesego, JJ Tabane.
Katika tamthilia ya Isidingo, Lesego alikuwa akiigiza kama  Lettie Matabane ambaye alikuwa akikumbwa na dhoruba nyingi.
Muigizaji huyo amemuacha mama yake mzazi, Ivy Skhosana na kaka zake wawili ambao ni Andile Skosana na Moemise Motsepe kwa upande wa familia yake.
Kwa mujibu wa mtayarishaji wa tamthilia hiyo kupitia kampuni ya SABC, waigizaji wenzake walijikusanya nyumbani kwao Kaskazini mwa Soweto ambapo walitarajiwa kujadili mipango ya mazishi.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Lesego mahala pema peponi. Apumzike kwa amani.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE