Mkali wa Hip Hop Tanzania anyemiliki tuzo moja ya wimbo bora wa Hip Hop 2012 - 2013 Nay wa mitego, ameweka wazi zamila yake ya kumuunga mkono Waziri mkuu mstafu Edward Lowasa.
Akizungumza leo Nay wa Mitego amesema
baada ya kumuimba Lowassa katika wimbo wake Salamu Zao, amepokea maoni
kutoka kwa vijana kuwa Lowassa ndiye kiongozi atakayeifaa Tanzania.
“Nikizungumzia kuhusu Lowassa yaani kila
mtu anam-support,kwasababu hata ukiangalia comment za kwenye Instagram
kila mtu anamadmire. Mimi sio mwanasiasa na wala siwezi siasa lakini
ni mtu ambae namkubali sana .Mimi namkubali sana na kama ikiwezekana
tukatuma maombi pia awepo kwenye wagombea Urais wa 2015,sijui kama yeye
yupo na plan hiyo lakini vijana na mimi tumetokea kumwelewa sana na
nimegundua watu wengi wapo nyuma yangu,”amesema Nay wa Mitego
0 MAONI YAKO:
Post a Comment