A.MKAGUZI MSAIDIZI WA UHAMIAJI (Nafasi 70)
SIFA ZINAZOHITAJIKA
-Awe na Shahada ya Kwanza au Stashahada ya Juu kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali katika fani zifuatazo:
Sheria, Uchumi, Biashara, Utawala, Uandishi wa Habari, Ualimu, Usafirishaji, Raslimali Watu, Sayansi ya Kompyuta, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Takwimu, Uchapaji, Uhandisi Majengo na Uhandisi Mitambo.
-Awe na umri usiozidi miaka 35
MAJUKUMU NA KAZI ZA KUFANYA
-Kusimamia doria sehemu za Mipakani, Bandarini, Vituo vya Mabasi, Treni na sehemu zenye vipenyo vya kuingia na kutoka nchini vikiwemo vya majini
-Kusimamia shughuli za upelelezi, kuandaa Hati ya Mashitaka na kuendesha mashitaka
-Kutoa na kupokea fomu mbali mbali za maombi ya Hati za Uhamiaji
-Kufanya Ukaguzi wa Mwanzo wa Maombi mbalimbali
-Kuagiza ufunguaji wa Majalada ya watumiaji
-Kupokea na kukagua Hati za Safari, Fomu za Kuingia na Kutoka Nchini
-Kuidhinisha malipo mbalimbali ya huduma za Uhamiaji kwa wanaostahili
-Kutunza kumbukumbu za ruhusa za watu wanaoingia na kutoka nchini
-Kukusanya, kusimamia na kutunza takwimu za Uhamiaji na Uraia
-Kuandaa majibu ya maombi yote ya huduma za uhamiaji yaliyokubaliwa au kukataliwa
Zaidi ingia: ajirazetu.com
0 MAONI YAKO:
Post a Comment