Hata hivyo, Gazeti la The Sun la juzi Jumapili lilikanusha kutaka
kuandika stori hiyo, lakini bado mlinzi wa kushoto wa England na Chelsea, Ashley Cole akawahi kukanusha kwamba alikuwa hahusiki na kashfa hiyo.
Cole ameimiliki nafasi ya ulinzi upande wa kushoto tangu Machi 2001
na ndiye mchezaji wa pembeni aliyecheza mechi nyingi zaidi katika kikosi
cha timu ya taifa ya England.
Na kama kutakuwa na ukwlei wowote katika habari hiyo ni wazi kwamba
hilo litakuwa pigo jingine kwa mchezaji huyo ambaye kwa sasa anahaha
kupata namba hiyo hiyo aliyoitawala muda mrefu katika kikosi cha Chelsea
na hivyo hiyo kuwa nuksi nyingine inayomuandama mchezaji huyo.
Mashabiki wengi waliamini kwamba Cole alikuwa anahusika na kashfa hiyo.
Mwingine aliyeonekana kuhisiwa katika kashfa hiyo ni mlinzi kinda,
Luke Shaw ambaye ameanza kuichezea timu ya taifa ya England katika
pambano la kirafiki dhidi ya Denmark Machi 8 mwaka huu. Hata hivyo wote wawili wametumia mitandao yao ya mawasiliano kukanusha uwepo wa habari hiyo.
Cole aliandika katika mtandao wake akisema ‘strictly chicks only’,
akimaanisha anapenda wasichana tu, wakati Shaw aliandika kwa kusema ‘Si
mimi’. Cole alikuwa katika ndoa na mwanamuziki maarufu wa Kundi la Girls
Aloud, Cheryl Cole
ambaye pia aliwahi kuwa jaji wa michuano ya kusaka vipaji ya X Factor
lakini ndoa yao ikavunjika mwaka 2010 kutokana na kile kilichodaiwa kuwa
Cole hakuwa mwaminifu katika ndoa hiyo.
Uvumi ulitanda Jumamosi usiku iliyopita katika mitandao ya kijamii
kwamba The Sun la Jumapili lingemtaja mchezaji mmoja katika kikosi cha
kocha Roy Hodgson ambaye anahusika na kashfa ya ushoga.
SOURCE: MWANASPOTI
SOURCE: MWANASPOTI
0 MAONI YAKO:
Post a Comment